Kila la kheri Yanga SC Botswana dhidi ya Township Rollers FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 13, 2018

Kila la kheri Yanga SC Botswana dhidi ya Township Rollers FC.


Ushindi wa Yanga SC 3-1 dhidi ya Stand United umeipa Yanga pointi tatu ambazo zinaifanya ifikishe pointi 46 na kuifikia Simba SC licha kwamba wekundu wa Msimbazi wanaendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Ally Ally (alijifunga) dakika ya saba, Ibrahim Ajibu akafunga goli la pili dakika tano baadaye, Obrey Chirwa ameifungia Yanga SC bao lililokamilisha ushindi wa Yanga . Goli pekee la Stand United limefungwa na Mayanga dakika ya 83.

Aidha kikosi cha Yanga SC kimeondoka usiku wa jana March 12, 2018 kuelekea Gaborone, Botswana, kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC.

Yanga SC imeondoka na msafara wa wachezaji 20 pamoja na viongozi 11 kuelekea Botswana ambapo mchezo huo utapigwa Machi 17 2018.

Katika mechi ya awali iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Yanga SC ilikubali kichapo cha mabao 2-1, hivyo sasa watalazimika kushinda zaidi ya mabao mawili, iwe 2-0, 3-0 au 4-1 ndiyo wataweza kusonga mbele.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad