Ajali ya Basi Thailand yaua 18. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 22, 2018

Ajali ya Basi Thailand yaua 18.

Watu 18 wamefariki dunia na wengine thelathini na watatu baada ya Basi la kukodi linalobeba watalii kuanguka katika eneo la milima Kaskazini Mashariki mwa Thailand.

Kituo cha luninga cha PBS kimetangaza kuwa ajali hiyo ilitokea katika jimbo la Nakhon Ratchasima.

Taarifa za kituo hicho zimesema abiria wa basi walikuwa wakirejea katika jimbo la Kalasin kutoka safari ya mbali wakielekea katika jimbo la Chanthaburi, lililo mpakani mwa nchi ya Cambodia. 

Takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinaonesha kuwa Thailand inashika nafasi ya pili duniani kwa idadi kubwa ya vifo vya ajali za barabarni baada ya nchi ya Libya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad