Yanga SC yaibutua Majimaji FC VPL 2017/2018. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 15, 2018

Yanga SC yaibutua Majimaji FC VPL 2017/2018.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji FC ya Songea kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara uliomalizika jioni ya Jana February 14,2018.

Baada ya mchezo wa huo ambao ulikuwa ni wa kiporo leo February 15,2018 vinara Simba SC wanatarajiwa kushuka kwenye dimba la Kambarage Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

Yanga SC ambayo imeshinda mchezo wake wa sita mfululizo imeendelea kupigania kutetea taji lake ambapo sasa imefikisha alama 37 nyuma ya Simba SC yenye alama 41 kwenye msimamo wa ligi.
Mabao ya Yanga SC yalifungwa na nyota wake Obrey Chirwa, Emmanuel Martin na Tshishimbi Kabamba aliyefunga mawili na kuifanya sasa timu hiyo ikamilishe ushindi wa tano katika michezo ya Ligi kuu ya hivi karibuni na sita ukijumlisha na michuano ya kimataifa.

Baada ya ushindi huu Yanga SC inatarajiwa kuondoka nchini siku ya Jumapili kuelekea nchini Shelisheli kwaajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Februari 21 dhidi ya wapinzani wao St. Louis.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad