![]() |
Tido
aliyakana mashtaka yote ambapo Wakili Swai alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika na wakili wake Ramadhan Maleta, Tido aliiomba Mahakama hiyo
impatie dhamana ambapo Hakimu Nongwa alitoa masharti ya kumtaka Tido atoe
fedha taslimu Sh.Mil 444 ama mali isiyohamishika ya thamani hiyo, kuwa na
wadhamini wawili ambapo kila mmoja asaini bondi ya Sh. milioni 500 na hatakiwi
kutoka nje ya nchi bila kibali cha Mahakama.
Tido
ametimiza masharti hayo na kutoa hati ya mali yenye thamani ya Sh.Mil 444
pamoja na kuwa na wadhamini ambapo kesi imeahirishwa hadi February
23,2018.
TUJIKUMBUSHE.
Tido alikuwa
Mkurugenzi Mkuu wa TBC kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idhaa
ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).
Kwa kipindi
cha miaka mingi alikuwa akifanya kazi ya utangazaji wa radio ambapo alianza
Utangazaji mwaka 1969 akiwa Radio Tanzania Dar es Salaam, (RTD), baadaye
akafanya kazi Kenya, halafu Uingereza na hatimaye akarejea tena RTD kabla ya
kuwa TBC.
Kwa sasa
Tido Muhando ni Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media.
Chanzo- /globalpublishers.
|
Friday, January 26, 2018

Tido Mhando kortini kwa Uhujumu Uchumi.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment