Taswira Picha George Weah Aapishwa kuwa Rais Liberia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 23, 2018

Taswira Picha George Weah Aapishwa kuwa Rais Liberia.

Rais Weah alipokuwa anakula kiapo mjini Monrovia.

Nyota wa zamani wa Soka Duniani, George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe January 22, 2018  iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.

Weah amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Bi.Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.

Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.

Akihutubia baada ya kula kiapo, Weah amesema: Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi.”

“Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu, lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu.”– George Weah
Mambo saba muhimu kumhusu George Weah:

  • Alizaliwa mnamo 1 Oktoba, 1966, na akalelewa katika mtaa wa mabanda Monrovia
 
  • Alinunuliwa na Arsene Wenger kuchezea Monaco kutoka klabu ya Tonnerre Yaoundé ya Cameroon
 
  • Alichezea Monaco mechi yake ya kwanza 1987, na baadaye akachezea AC Milan, Paris Saint-Germain na Chelsea
 
  • Ndiye Mwafrika pekee aliyewahi kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani ya Fifa
 
  • Aliwania urais mara ya kwanza 2005, na akashindwa na Ellen Johnson Sirleaf
  • Alifuzu na shahada ya biashara kutoka chuo kikuu kimoja cha Marekani, baada ya kudaiwa hakuwa na elimu 
 
  • Alichaguliwa rais Desemba 2017
      

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad