Taswira Picha 21 za Wana Ngara walipofurahi na Kombe la Kumuyange FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 20, 2018

Taswira Picha 21 za Wana Ngara walipofurahi na Kombe la Kumuyange FC.

Wadau wa Ngara Mjini na Pozi lao.

Kombe hilo la Ubingwa wa Mkoa wa Kagera 2017/2018 lilitembezwa katika maeneo ya Kumunazi,Benaco,Rusumo,Mshikamano,Nyakisasa,Nyamahwa,Rulenge,Djululigwa,Kabanga,Mabawe,Ngara Mjini na Kumuyange ambapo pamoja na kuelezea mafanikio ya Kumuyange FC Wanangara walipata nafasi ya kupiga picha na Kombe hilo ambalo Kumuyange FC alilishinda baada ya kumvua Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1 Jana January 14,2018 uwanjani Kaitaba,Bukoba.


Hawa ni Wadau wa Kabanga.


Hawa ni Wadau wa Rulenge wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Chama cha Soka wilaya ya Ngara NDFA-Mwl Mashaka Makemba.


Madau wa Rulenge Mama Helena Adrian alitoa wito kwa Vijana wa Ngara kujitokeza kucheza soka ili kuonesha vipaji vyao na Kombe hilo la Ubingwa wa Mkoa wa Kagera liwe chachu kwa Viongozi na Wadau kupambana ipasavyo kufikia mafanikio katika Michezo wilayani.


Mwenyekiti wa Timu ya Kumuyange FC-Ezron Nyamunda na Mdau wa Mabawe wakilionesha Kombe kwa Wana Mabawe.


Mama yetu wa Mabawe kwa raha zake na Kombe .


Hawa ni Wadau wa Rulenge


Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Ngara Godard na furaha ya Ubingwa wa Kumuyange FC.


Viongozi wetu wa Kumuyange na Pozi la Picha na Kombe letu.



*Tumejipanga kufanya vyema Ligi Taifa ya Mabingwa wa Mkoa, Kombe la Shirikisho la Azam sambamba na kuhakikisha Watanzania wanalitambua soka la Ngara, kitaifa *Mwenyekiti wa Kumuyange FC - Ezron Nyamunda -Pichani Kulia.

Ubingwa wa Kumuyange FC unawafanya  kuandika rekodi ya kuubeba Ubingwa wa Mkoa bila kupoteza mechi yake hata moja,ikishinda zote toka hatua ya makundi na ligi ndogo ,ikifunga Jumla ya magoli 34,Mchezaji wake Denis Msuva akipiga Hat Trick 4 na kuibuka mfungaji bora na wmeubeba Ubingwa kwa kujikusanyia Pointi 9.


Wadau wa Kabanga na raha ya Ubingwa wa Kumuyange FC.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad