Jengo la
Shule Binafsi.
Wizara ya
Elimu nchini imezionya shule zisizo za kiserikali zinazofukuza au kuwahamisha
wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufauli wa shule kuacha kufanya
hivyo mara moja.
Aidha
kupitia waraka wa Elimu Namba 7 wa Mwaka 2004, wizara hiyo pia imewataka wazazi
ambao watoto wao walikutana na adha hiyo kuwarejesha katika shule hizo na shule
itakayokaidi itachukuliwa hatua za kisheria kwa kufutiwa leseni ya usajili au
kufungiwa kabisa.
Wanafunzi
ambao wamedaiwa kukutana na sakata hilo ni pamoja na wale wanaofanya mitihani
ya darasa la Nne na Kidato cha pili.
Taarifa hiyo
imeongeza kuwa, inadaiwa kuwa wapo walimu wakuu wa shule kadhaa wanaofikia
hatua ya kuwatuhumu wanafunzi hao kwa makosa ya utovu wa nidhamu na kuwaeleza
walezi na wazazi kuwahamisha ama warudie darasa wanafunzi hao.
Kwa mujibu
wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Kamishna wa Elimu, Dkt. Edicome Shirima, shule
zote zilizofanya hivyo zimetakiwa kuwaruhusu wanafunzi hao kurejea shuleni
Januari 20, mwaka huu ili waendelea na madarasa waliyopaswa.
Aidha wizara
hiyo ya elimu imewakumbusha wamiliki na waendeshaji wa shule wote kuzingatia
sheria, kanuni na miongozo ya elimu nchini.
SOMA TAARIFA
RASMI HAPA CHINI.
|
No comments:
Post a Comment