Ajali ya Basi la Saratoga yaua Mtu Mmoja akipatiwa Matibabu Hospitali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 18, 2018

Ajali ya Basi la Saratoga yaua Mtu Mmoja akipatiwa Matibabu Hospitali.

Majeruhi mmoja kati ya saba waliopata ajali ya Basi la Saratoga iliyotokea January 17,2018 katika kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Sabina Daudi Kimoli (49) amefariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Biharamulo.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Matondane Paul amesema marehemu huyo aliumia kichwa na damu kuvujia ndani ya ubongo na alifariki jana saa5 usiku na kwamba mwili wa marehemu utaendelea kuhifadhiwa hadi ndugu na jamaa watakapokuja kuuchukua kuelekea nyumbani wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Paul amesema majeruhi wengine sita wamepata matibabu na kuruhusiwa ambapo mwili wa marehemu mwingine aliyepoteza maisha katika ajali ya kwanza iliyotokea kata ya Nyantakara jumapili January 14,2018 haujatambulika na marehemu huyo wa jinsia ya kike anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 70.

Amesema pia katika ajali hiyo iliyohusisha vifo vya watu 11 marehemu 10 walitambuliwa na ndugu na miili ilichukuliwa kwa ajili ya mazishi na kati ya majeruhi watano mmoja alisafirishwa hadi Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi na wengine walikwenda kutibiwa karibu na majumbani mwao kwenye maeneo walikotokea.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Agustino Olomi amesema marehemu Sabina Daudi Kimoli alipata ajali katika basi la Saratoga lenye namba za usajili T. 114 AAG iliyokuwa ikitokea Mwanza kwenda Kigoma.

Amesema basi hilo liligongana na roli lenye namba za usajili T803 BHQ na tela lenye namba T 281BGQ na kwamba madereva wa magari hayo wanashikiriwa na Jeshi la Polisi kwa upeleleza zaidi kabla ya kufikishwa kwenye mkondo wa sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad