Matokeo ya Mechi za EPL 201/2018 December 2, huku Man United ikiiadhibu Arsenal 3-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 03, 2017

Matokeo ya Mechi za EPL 201/2018 December 2, huku Man United ikiiadhibu Arsenal 3-1.

Kikosi cha Jose Mourinho kilipunguzwa na kuwa na wachezaji 10 katika dakika za mwisho baada ya Paul Pogba kupewa kadi nyekundu kwa kucheza visivyo na walisaidiwa na kipa wao David de Gea katika mechi yote. 

Lakini licha ya hayo Arsenal iliadhibiwa mapema na Antonio Valencia wakati alipopata pasi mbaya ilioandaliwa na beki wa Arsenal Koscielny na kuweza kuiweka kifua mbele Manchester United kabla ya Jesse Lingard kufunga la pili baada ya kumpkoonya mpira Shkodran Mustafi.
Jesse Lingard akishangilia baada ya kuifungia Manchester United mabao mawili dakika za 11 na 63 ikiwalaza wenyeji, Arsenal 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates, London. 

Bao lingine la Man United iliyomaliza pungufu baada ya kiungo wake, Paul Pogba kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 74 kwa kumchezea tafu Hector Bellerin, lilifungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 49 akimalizia pasi ya Aaron Ramsey
Manchester United Waliiadhibu safu ya ulinzi ya Arsenal na kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika uwanja wa Emirates tangu mwezi Januari katika mojawapo ya mechi za ligi ya Uingereza msimu huu.

HAPA NI MATOKEO YOTE YA MECHI ZA JANA JUMAMOSI.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad