Hawa
wanadaiwa wamevamia vyanzo vya maji !! Inadaiwa na viongozi pia kuwa hili ni
eneo la wafugaji !! Serikali ya kijiji iliwapa ardhi kaya zile waishi na
walime. Wanazo stakabadhi! Ipo sintofahamu hapo,
Msaada wa
hali na mali ikiwemo wa kisaikolojia unahitajika kwa waathirika wa tukio hili
hususani akina mama, watoto,, na wanachi wote kwa ujumla ambao kwa sasa,
wanashindwa waende wapi au wafanye nini. Mvua za masika zimeanza na wananchi
hawa hawana pa kulala.. na hawana chakula....
|
Tukio hili linakuja sasa kufuatia Mkuu wa Wilaya Karagwe ,Bw.Godfrey Mheruka kuanzisha operation ya kuondoa wavamizi wa vyanzo vya maji na uchafuzi wa mazingira. |
DC Mheruka
akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo, ameanzisha operation hiyo
ya kuondoa wananchi waliovamia katika vyanzo vya maji na kuharibu mazingira
ambapo wakiwa katika kijiji cha Chabuhora katika Kata ya Nyakabanga, waliwakuta
wananchi wanaodaiwa kuvamia vyanzo vya
maji na kuweka makazi na kuanzisha shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo,
kukata miti hovyo, kuchoma mkaa pamoja na uwindaji haramu.
Aidha waliamua
kuteketeza makazi ya wananchi hao na kuwataka warudi katika makazi yao ya
zamani ikiwa ni pamoja na kuwaagiza Watendaji wa Kitongoji hadi Wilaya
kusimamia zoezi hilo kuhakikisha hawarudi katika maeneo hayo kabla hatua kali
za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
|
Habari/Picha
Na Joseph Sekiku.
|
No comments:
Post a Comment