
![]() |
|
Abiria
wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka (UDART) wamekwama Kimara kutokana
na kukosekana huduma kulikosababishwa na ajali iliyotokea Shekilango, Ubungo leo September 14,2017 Asubuhi.
Vituo vya
UDART vilivyoko Mbezi Mwisho hadi Ubungo vimefurika abiria baadhi wakiamua
kutafuta usafiri mbadala.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano cha UDART, Deus Bugaywa amesema gari moja liligonga
lingine kwa nyuma hivyo kusababisha barabara kutopitika.
Bugaywa
amesema baada ya mabasi ya UDART yaliyogongana kuondolewa, hivi sasa
wanachofanya ni kuhakikisha abiria wote walio vituoni wanapata usafiri.
|







No comments:
Post a Comment