Simon Msuva aipa Taifa Stars magoli 2 dhidi ya Botswana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 02, 2017

Simon Msuva aipa Taifa Stars magoli 2 dhidi ya Botswana.

Goli la kwanza la Taifa Stars dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA leo September 2,2017 limefungwa dakika ya tano (5) kipindi cha kwanza ampapo Msuva alimalizia kazi pasi safi ya Mzamiru Yassin huku bao la pili likifungwa dakika ya 61 kipindi cha pili ambapo Kichuya alifanya kazi ya ziada iliyomaliziwa kwa ustadi na Msuva.

Simon Msuva pichani amesema magoli mawili aliyofunga kwenye mechi dhidi ya Botswana yatamsaidia kujiamini katika klabu yake ya Difaa El Jadid pindi atakaporejea Morocco.

Msuva amecheza katika kiwango cha juu dhidi ya Botswana na kufanikiwa kutumia vizuri nafasi alizozipatakupachika mabao yaliyoipa Taifa Stars ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wa nyumbani.

Magoli mawili niliyofunga kwenye timu ya taifa yataniongezea kujiamini na kwenda kufanya vizuri kwenye klabu yangu lakini nitaendelea kuaminika kwenye timu kwa sababu unapocheza kwenye timu ya taifa na kufunga wanaona huyu mchezaji anaweza kutusaidia,” Simon Msuva.

Taifa Stars ilipata ushindi wa magoli 2-0  mwezi March 25, 2017  katika ushindi ambao imeupata tena leo Septmber 2, 2017 yote ikiwa ni michezo ya kirafiki ndani ya miezi saba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad