Madiwani
wahalmashauri mbili za Wilaya ya Geita jana Jumatano walitanga mgogoro na GGM
wakishinikiza kulipwa Dola 12 milioni za Marekani zinazotokana na ushuru wa
huduma kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.
Walitangaza
kuzuia magari ya mgodi kwa kufunga
barabarana pia kufunga maji yanayoingia mgodini kutoka Ziwa Victoria.
|
GGM
iliwatangazia wafanyakazi wake jana kutofika kazini leo kutokana na mgogoro
huo.
Polisi hivi
sasa wameimarisha ulinzi kwenye maeneo ya Nungwe uliko mradi wa kusambaza maji
mgodini, eneo la uwanja wa ndege na geti la kuingia mgodini.
Mkuu wa
Wilaya ya Geita, Herman Kapufi na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma
wameingia mgodini baada ya madiwani na wananchi kutawanywa.
|
CHANZO:
MWANANCHI
|
No comments:
Post a Comment