Picha-Singida United watambulisha Basi lao Jipya aina ya Dragon. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 04, 2017

Picha-Singida United watambulisha Basi lao Jipya aina ya Dragon.

Uongozi wa Klabu ya Singida United, imetoa basi lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 350 litakalotumiwa na wachezaji pamoja na benchi lao la ufundi katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania bara wa 2017/2018.

Kikosi a Singida United kimerejea Ligi Kuu Bara Msimu huu na Leo Jumanne July 4, 2017 kitaingia kambini mjini Mwanza chini ya Kocha wa zamani wa Yanga SC, Hans van der Pluijm ndiye kocha anayekinoa kikosi hicho ambacho kinadhaminiwa na SportPesa.
Muonekano wa gari la Singida United linaloratajiwa kutumiwa na wachezaji wa timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu.


Katika basi hiyo, Singida United imeweka picha za Rais wa timu hiyo, Mwingulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na picha ya mmiliki wa timu, Yusuf Mwandami.

Meneja wa klabu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kulitambulisha basi lao jipya litakalotumika kwa safari za ndani za timu ya Singida United.
Basi hilo aina ya Dragon lenye thamani ya Sh 350 milioni limezinduliwa rasmi na litaanza kutumika katika safari za timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu 2017/2018.

Post Bottom Ad