Ujerumani waitandika 3-2 Australia-FIFA Kombe la Mabara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 20, 2017

Ujerumani waitandika 3-2 Australia-FIFA Kombe la Mabara.

Mabingwa wa Dunia,Ujerumani wameanza vyema mechi yao ya Kundi B la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara iliyochezwa huko Fisht Stadium, Mjini Sochi, Nchini Russia, kwa kuibwaga Australia mabao 3-2.

Ujerumani waliongoza bao 2-1 kwa goli la Lars Stindl, dakika ya 5, na Julian Draxler kwa Penati ya dakika 45, wakati Australia wakifunga Bao lao dakika ya 41 ambalo alifunga Tom Rogic.

Ujerumani katika kipindi cha pili walifunga goli la 3 Dakika ya 48 Mfungaji akiwa Leon Goretzka lakini Australia wakapata bao la Pili dakika ya 58 kupitia Tomi Juric.

Leo Jumanne June 20,2017 ni Mapumziko na Jumatano June 21,2017 kuna mechi mbili  za Kundi A ambapo Wenyeji Russia wataanza na Portugal na kufuatia Mexico na New Zealand.

Post Bottom Ad