Uchaguzi Mkuu TFF wafikisha Wagombea 62, Mwisho wa Zoezi la Fomu Leo June 20,2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 20, 2017

Uchaguzi Mkuu TFF wafikisha Wagombea 62, Mwisho wa Zoezi la Fomu Leo June 20,2017.

Wakati Leo Jumanne Juni 20, 2017 itakuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wagombea 62 tayari wamejitokeza.

Wanafamilia hao ni wale waliojitokeza kuanzia Ijumaa iliyopita Juni 16, mwaka huu wakiongozwa na Jamal Malinzi aliyekuwa wa kwanza kuchukua fomu kati ya wagombea tisa walioomba nafasi hiyo.

Fomu hizo zinachukuliwa na kurejeshwa katika ofisi za TTF, Karume jijini Dar es Salaam na Uchaguzi wa TFF utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Mbali ya Malinzi, wengine waliochukua fomu hizo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela na Ally Mayay wakati waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais wako Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani na Robert Selasela.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

Soloum Chama

Kaliro Samson

Samwel Daniel

Leopold Mukebezi

Abdallah Mussa

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

Vedastus Lufano

Ephraim Majinge

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

Benista Rugora

Mbasha Matutu

Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

Omari Walii

Sarah Chao

Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

John Kadutu

Issa Bukuku

Abubakar Zebo

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

Kenneth Pesambili

Baraka Mazengo

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya na Iringa;

Elias Mwanjala

Cyprian Kuyava

Erick Ambakisye

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

James Mhagama

Golden Sanga

Vicent Majili

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

Athuman Kambi

Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida; 

Hussein Mwamba

Mohamed Aden

Musa Sima

Stewart Masima

Ally Suru

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

Charles Mwakambaya

Gabriel Makwawe

Francis Ndulane

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga;

Khalid Mohamed

Goodluck Moshi

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam;

Emmanuel Ashery

Ayoub Nyenzi

Saleh Alawi

Shaffih Dauda

Thabit Kandoro

Abdul Sauko

Peter Mhinzi

Ally Kamtande

Said Tully

Mussa Kisoky

Lameck Nyambaya

Ramadhani Nassib

Aziz Khalfan

GHARAMA ZA KUCHULIA FOMU.
 1. Rais TSHS 500,000/=
 2. Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
 3. Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/-
SIFA ZA WAGOMBEA.
 1. Awe raia wa Tanzania.
 2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha   Elimu ya Sekondari).
 3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
 4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
 5. Awe na umri angalau miaka 25.
 6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
 7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
 8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi (10:00) jioni
..……………………………………………………………………………………………..
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

Post Bottom Ad