Taswira Picha-Adakwa akitaka kuingiza simu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 20, 2017

Taswira Picha-Adakwa akitaka kuingiza simu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salaam.

Jeshi  la Magereza Jumapili June 18,2017 limemkamata kijana mmoja aitwaye Ramadhani Nombo –Pichani-akiwa na simu tano alizozificha kwenye mapande ya nyama aliyokuwa amepelekea ndugu yake/zake  mahabusu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi hilo, hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha Mahakamani mtuhumiwa huyo.

Kutokana na umakini wa askari wetu,  mara tu alipofika Keko na kuomba kuwaona ndugu zake walio mahabusu na kuwapa chakula walibaini kwamba ndani yake kuna simu” imesema taarifa hiyo. 

Haikutajwa nyama na hizo simu alikuwa anapalekewa  mahabusu gani hapo gerezani.

Taarifa zinasema kimsingi kijana huyo amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria ya Magereza sura ya 56 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ambayo inakataza mtu yeyote kuingiza magerezani kitu chochote kisichoruhusiwa.
 Mtuhumiwa Ramadhani Nombo akiwa amebeba mapande ya nyama ambayo yanatuhumiwa kuwa na simu tano ndani yake.

Kifungu hicho kinatamka bayana kwamba endapo ikithibitika mtu yeyote amekamatwa na kuingiza kitu chochote ambacho hakiruhusiwi kuingizwa gerezani, atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita (6) gerezani au faini au vyote kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad