Taswira Picha Ajali ya Basi la Superfeo wilayani Songea na kuua Mtu mmoja. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 25, 2017

Taswira Picha Ajali ya Basi la Superfeo wilayani Songea na kuua Mtu mmoja.

Kampuni ya Mabasi ya Superfeo inayosafirisha abiria toka Jijini Mbeya hadi mjini Songea imepata ajali katika eneo la Hangagadinda wilayani Songea na kuua mtu mmoja ambaye alikuwa ni kondakta wa basi hilo.

Meneja huduma wa Kampuni hiyo Fransisi Sengo anasema ni siku moja tu imepita baada ya ajali nyingine ya Superfeo kutoka Mbeya kuja Songea kupata ajali juzi katika kijiji cha Mbangamawe wilayani Songea na kuua Dereva wa basi hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya ya Songea ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya ya Songea,Bw. Pololet Kamando Mgema ametembelea eneo la ajali ambapo Inadaiwa ajali hiyo ilisababishwa na Dereva ambaye alikuwa anaongea na simu huku anaendesha gari. 

Bw.Mgema ameagiza vyombo vya dola kufuatilia tabia za madereva ikiwa ni pamoja na kuwapima viwango vya ulevi ili kupunguza ajali zisizo za lazima.
Habari/Pichakwa Hisani ya RSA TANZANIA(Road Safety Ambassadors)

Post Bottom Ad