Kisa Nitunzie Siri ,Yamvuta Mo Music kufanya Collabo na Kundi la Wapancras. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 27, 2017

Kisa Nitunzie Siri ,Yamvuta Mo Music kufanya Collabo na Kundi la Wapancras.

Kundi la Wapancras.

Mwamauziki  Mo Music amevutiwa na wimbo wa Nitunzie Siri ulioimbwa na kundi la Wapancras kutoka Kanda ya Ziwa, linaloundwa na Wasanii Mecrass na Payus na hivyo kukubali kusikika kwenye wimbo mpya ujao wa kundi hilo.

 Akizungumza na Mtandao huu wa Mwana wa Makonda ,Msanii Mecrass amesema kuwa “Mo Music alitembelea studio za Vibe Nation na aliposikiliza wimbo wetu wa Nitunzie Siri akavutiwa kufanya kazi na sisi hivyo hatukusita kuitumia nafasi hiyo”. 

Licha ya hilo,kwa sasa Wapancras wapo  pia  kwenye mchakato wa kufungua studio yao mpya iitwayo Alive Music.
Mo Music.

Wapenzi na mashabiki wetu watarajie ngoma kali hivi karibuni tukiwa na mkali wa Basi Nenda, Mo Music.

Tulikaa kimya kidogo kwa ajili ya kujikita kwenye ufunguzi wa studio yetu mpya lakini pia kuziachia nafasi ngoma zetu ziendelee kufanya vizuri sokoni”. Amesema Mecras.

Wapancras wamesema wimbo huo utatoka hivi karibuni ambapo umetengenezwa katika studio za Vibe Nation.

Post Bottom Ad