VPL 2016/2017– Yanga SC na Azam FC vitani Leo huku Kagera Sugar na Simba SC kesho Kaitaba-Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 01, 2017

VPL 2016/2017– Yanga SC na Azam FC vitani Leo huku Kagera Sugar na Simba SC kesho Kaitaba-Bukoba.

Azam FC v Yanga SC.

Ligi Kuu soka Vodacom Tanzania bara 2016/2017 inarejea tena kwa kishindo Jumamosi hii Aprili Mosi,2017  kwa Mechi 3 na kubwa ni ile inayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ,Mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa na shughuli na Azam FC.

Mechi nyingine za hiyo Jumamosi, ambazo hasa nyingi ni vita za kutoshuka Daraja, ni huko Songea kati ya Maji Maji FC na Toto Africans wakati nyingine ni Mjini Mbeya kati Mbeya City na Ruvu Shooting.
Simba SC wakiwa Bukoba.

Kesho;Jumapili April 02,2017 zipo Mechi 4 na Macho Kodo ni huko Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba kati ya Kagera Sugar, walio nafasi ya 4, wakiwavaa Vinara Simba SC.

Mbio za Ubingwa zinaongozwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wenye pointi 55, wakifuatiwa na watetezi wa taji, Yanga SC wenye pointi 53 baada ya timu zote kucheza mechi 24 na wikiendi hii miamba hiyo ya soka nchini itamenyana na timu zinazowafuatia kwa ubora katika Ligi Kuu, Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na Kagera Sugar iliyo nafasi ya nne kwa pointi zake 42, kufuatia kila timu kucheza mechi 24.

Msimamo VPL 2016/2017.
Mechi nyingine za Jumapili ni Jijini Dar es Salaam kati ya African Lyon na Stand United, Mjini Mbeya ni Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar na huko Mwadui Complex, Shinyanga ni Mwadui FC na JKT Ruvu.

VPL – LIGI KUU VODACOM

Jumamosi Aprili 01,2017.

Yanga SC v Azam FC

Maji Maji FC v Toto Africans

Mbeya City v Ruvu Shooting

Jumapili Aprili 02,2017.

Kagera Sugar v Simba SC

African Lyon v Stand United

Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar

Mwadui FC v JKT Ruvu

Post Bottom Ad