Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukabidhiwa taarifa
ya tume ya kuchunguza suala la Faru John na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa
Samwel Manyele, Ofisini kwake jijini Dar es salam Machi 27, 2017.
Mengine ni
uchukuaji holela wa sampuli za wanyama pori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha
nje ya nchi; migongano ya kimaslahi kati ya watumishi waliolenga kusimamia
taratibu na wale wenye kusimamia maslahi binafsi na uwepo wa taasisi nyingi
zenye mamlaka sawa juu ya masuala ya uhifadhi wa wanyamapori.
“Pamoja na
kwamba mawasiliano yanaonyesha zoezi hilo liliridhiwa na Wizara,hapakuwepo na
kibali rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori cha kuruhusu kumhamisha Faru
John kutoka NCAA kwenda Grumeti,” amesema Prof.Manyele katika ripoti yake.
Akizungumzia
kuhusu uchukuaji holela wa sampuli za wanyama pori kwa lengo la utafiti na
kuzisafirisha nje ya nchi, Prof. Manyele amesema kumbukumbu za watafiti na aina
ya sampuli wanazochukua haziwekwi vizuri
na kwamba tume inashauri TAWIRI na TANAPA wapewe msisitizo juu ya
umuhimu wa kuzingatia majukumu yao.
Amesema kuna
umuhimu wa kudhibiti watafiti na tafiti ili kulinda taarifa muhimu za vinasaba
vya wanyamapori (Genetic information) dhidi ya mataifa mengine. “TUME inashauri
maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ianzishe kitengo cha Sayansi Jinai na
Uchunguzi wa Vinasaba vya Wanyamapori (DNA Forensic Wildlife Laboratory) ili
Serikali na vyombo vyake iweze kufanya maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata
ushahidi wa kimahakama katika kesi za jinai zinazohusu wanyamapori (Expert
Witness).
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kusomewa ripoti huyo, Waziri Mkuu aliishukuru
timu ya uchunguzi iliyokuwa chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi
iliyoifanya ikiwemo kuainisha udhaifu uliokuwemo ndani ya Wizara ya Maliasili
na Utalii na taasisi zake.
“Ofisi yangu
itaipitia taarifa hii ambayo ni kubwa kiasi na kuifanyia kazi. Matokeo ya kazi
hiyo, tutayatoa hivi karibuni ili kuonyesha Serikali imeamua kufanya nini juu
ya mapendekezo yaliyotolewa.”
Alimtaka Mkurugenzi
Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande, afuatilie
mapendekezo yaliyoainishwa na tume hiyo na wayafanyie kazi mapema iwezekanavyo.
Waziri Mkuu
aliiunda tume hiyo Desemba 10, mwaka jana baada ya kupokea pembe mbili za faru
John na taarifa yenye nyaraka zilizotumika kumhamisha faru huyo. Hatua hiyo
ilifuatia agizo alolitoa Desemba 6,2016, akiwa ziarani mkoani Arusha, ambapo
alitoa siku mbili na kuutaka uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru John kutoka kwenye
hifadhi hiyo.
Alitoa agizo
hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro,
mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa
Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
|
Tuesday, March 28, 2017
Kifo cha FARU JOHN Kilitokana na Kukosa Matunzo.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment