Baada ya Kuachiwa:Lema na Sentensi zake Katika Mkutano Wake wa Kwanza –Arusha. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, March 11, 2017

Baada ya Kuachiwa:Lema na Sentensi zake Katika Mkutano Wake wa Kwanza –Arusha.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoka rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne.

Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.
Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamilisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.

Amewataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .

Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo jijini Arusha.
Mbali na Lema, mwingine aliyepata nafasi ya kuzungumza na umati huo uliojitokeza Jana ni mwanachama mpya wa chama hicho, muigizaji Wema Sepetu.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama mkoani humo akiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro.

Post Bottom Ad