Vita Dawa za Kulevya Kagera: Ngara na Biharamulo Watano wakamatwa kwa Kujihusisha na Kilimo cha Bangi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 24, 2017

Vita Dawa za Kulevya Kagera: Ngara na Biharamulo Watano wakamatwa kwa Kujihusisha na Kilimo cha Bangi.

Jeshi la polisi katika wilaya za Ngara na Biharamulo mkoani Kagera linawashikilia wakazi watano wa wilaya hizo kwa kujihusisha na kilimo cha bangi ambayo ni madawa ya Kulevya huku wakihusika kuharibu mazingira ya misitu.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kukamatwa kwa watu hao, ambao walikamatwa kwenye operesheni ya kukamata wanaojihusisha na kilimo cha bangi  wiki hii pamoja na watumiaji au wafanya biashara wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Kagera .

Kamanda Olomi aliwataja waliokamatwa kwenye wilaya hizo ni Fabian Kasigo (45), mkazi wa Kazingati, Ndaluhekeye Chiza (37),Nestory Kachukuzi 42), Renatus James (44) Khalid John (33) wakazi wa wilaya ya Ngara na James Maliatabu (35) mkazi wa kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo.

Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele alisema katika msako wa kuwakamata wakulima wa bangi wilayani Ngara jumla ya mashamba ekari 20 yalibainika na wakulima wa zao hilo wanalilima katikati ya mapori wilayani humo

Mntenjele alisema wakulima waliokamatwa na kuhojiwa walidai wanauz zao hilo kati ya Sh15,000 hadi Sh 17 000 kwa wateja kutoka nchi jirani za Rwanda na Burundi na kwamba wanalima zao hilo wakikata miti kwenye vyanzo vya maji

Wanapolima bangi wanaiweka katikati ya mashamba ya mahindi na huwezi kutambua kwani wanatembea umbali mrefu katikati ya mabonde yanye vyanzo vya maji na kukata miti kisha kupanda kupanda bangi hiyo”Alinema Kanali Mntenjele

Alisema katika msako uliofanyika kwa siku tatu wilayani Ngara kata ya Ntobeye, Keza kiasi cha ekari 20 zilibainika, wanaolima zao hilo  wakiwatumia hata wahamiaji haramu kutoka mataifa jirani na wilaya hiyo wakiishi porini na kuletewa mahitaji ya chakula.
Aidha mkuu wa wilaya ya Biharamulo Saada Malunde alisema kata iliyofanyiwa msako kukamata wakulima wa bangi ni kata ya Nyantakara na Nemba ambapo mkulima mmoja James Maliatabu  (35) alikutwa  na shamba la bangi  ekari 10.

Alisema vita ya dawa za kulevya kwa maeneo ya vijijini ni utumiaji wa bangi ambapo pia kamati za mazingira katika vitego na idara za halmashauri zinatakiwa kuunga mkono serikali kuwataja na kuwakamata wanaojihusiha na biashara ya madawa ya kulevya ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

Pia baadhi ya wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama katika wilaya hizo walishauri serikali za vijiji na madiwani hata maafisa kata na tarafa kufanya zoezi la kuwasaka wakulima wa bangi kila mahali ili kutokomeza madawa ya kulevya kote nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad