Fursa ya Elimu Mwaka 2017-Moon Light Training Center Ngara/Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 03, 2017

Fursa ya Elimu Mwaka 2017-Moon Light Training Center Ngara/Kagera.

Taasisi ya MOONLIGHT  TRAINING  CENTER –NGARA/KAGERA  ni taasisi iliosajiliwa na serikali kupitia Mkufunzi mkuu Mkazi  wa mkoa na mkufunzi mkuu mkazi Taifa  kuendesha mafunzo ya elimu ya sekondari kupitia mpango wa Elimu masafa na ana kwa ana yaani -Open and Ditance Leaning (ODL)-katika ngazi mbalimbali ikiwemo mafunzo ya elimu ya computer na wanao hitaji kujiendeleza kitaaruma.

Taasisi ya MOON LIGHT  TRAINING CENTER inapenda kuwatangazia jamii yote ya Ngara na Maeneo jirani kuwa, Tunawakaribisha kujiunga katika program mbalimbali kama zinavyotolewa,

1.Masomo ya kidato cha kwanza na kidato cha pili (Qualified Test QT) .

Sifa:

1.   Awe amemalizadarasa la saba na anahitaji kupata elimu ya sekondari (hatujali umri wa mtu)

 2.Ambaye amepata elimu ya sekondari katika mfumo rasmi (kidato cha kwanza au cha pili) lakini hakufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili.

2.Masomo ya kidato cha tatu na kidato cha nne.

Sifa:   

1.Ambaye amefaulu mtihani wa maarifa (QT) wa Hatua ya I.

2.Ambayea mefaulu mtihani wa taifa wa kidato cha pili.

3.Ambaye anataka kurudia mtihani wa kidato cha nne.

3.Masomo kidato cha tano na kidato cha sita

      Sifa:

1.  Awe ameshafanya mtihani wa kidato cha nne na kupata angalau ufaulu wa C tatu na kuendelea.

2.Ambaye anataka kurudia mtihani wa kidato cha sita.

4.Masomo ya Computer katika hatua zote kwa mda wa miezi mitatu,sita na mwaka mmoja.

 Sifa: 

 Awe amemaliza darasa la saba nakuendelea.

 5.Masomo ya secretarial course kuanzia miezi sita mpaka mwaka mmoja.

   Sifa: 

Awe amemaliza kidato cha nne na kuendelea.

Taasisi ya elimu ya MOONLIGHT TRAINING CENTER inapatikana gorofa ya  kwanza katika jengo la TTCL Ngara karibu na ofisi za TRA Ngara,barabara ya kenyata.

Fomu za kujiunga zinapatikana kunzia sasa kwa gharama sh.5,000.

Ada na michango mingine imefafanuliwa katika fomu ya maombi ya kujiunga na taasisi yetu.

Tuna walimu wenye sifa na taaluma,vitabu na nyenzo za kufundishia rafiki kwa wanafunzi,tunakuhakikishia kukamilisha ndoto zako.

Kwa mawasiliano unaweza kuwasiliana nasi kupitia: 0758421849au 0686706350
au 0752776718 au 0717254988.

Mafunzo yameisha anza rasmi kuanzia tarehe 09 January 2017.

Wahi kuchukua fomu nafasi ni chache.

“Tunamulika na kufanikisha ndoto zako”

Wanafunzi wote watafundishwa computa kama somo bure.

KARIBU SANA, UPATE TAALUMA  KWA GHARAMA NAFUU NA YENYE TIJA KWA ZAMA HIZI  ELIMU KWANZA.

Post Bottom Ad