AFCON 2017: Cameroon Bingwa mara 5. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 06, 2017

AFCON 2017: Cameroon Bingwa mara 5.

Timu ya Taifa ya Soka ya Cameroon wameifunga Misri  magoli 2-1  hapo Jana February 05, 2017 huko Libreville, nchini Gabon na kutwaa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika –AFCON 2017  ikiwa ni katika Mashindano ya 31.

Hii ni mara ya kwanza kwa Cameroon kuifunga Misri katika Fainali 3 walizokutana nayo huko nyuma na hii ni mara yao ya kwanza kutwaa Ubingwa wa Afrika tangu Mwaka 2002 ilipokuwa mara yao ya 4 kuwa Bingwa.
Ushindi huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri, walifungwa fainali ya AFCON 2008 kwa kipigo cha goli 1-0 la Mohamed Aboutrika, lakini mwaka 1986 walipoteza tena mchezo wa fainali.

Sasa Cameroon wanakuwa wamechukua taji lao la tano la AFCON huku Misri bado wakiendelea kuwa wababe wa taji hili wakiwa na rekodi ya kulichukua mara saba.

Misri ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 22 Mfungaji akiwa Kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili, Wachezaji Wawili wa Cameroon walioanzia Benchi ndio waligeuza Mechi pale Nicolas N’Koulou aliposawazisha Dakika ya 59 na Vincent Aboubakar kuwapa ushindi Dakika ya 88.

Bao hizo ziliamsha nderemo na vifijo miongoni mwa Mashabiki 38,000 wengi wao wakiwa ni wa Cameroon.
NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA.

-Egypt-Mara 7

-Cameroon- Mara 5

-Ghana-Mara 4

-Nigeria-Mara 3

-Congo DR-Mara 2

-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad