Alisema
serikali kwa kutumia vyombo vyake, imejiridhisha kwamba hakuna hali mbaya ya
usalama, inayowakimbiza raia hao kutoka kwenye nchi zao na kwamba zaidi
imegundulika kuwa wengi wao wanakimbia kwa sababu za kiuchumi, kuja kutafuta
namna ya kuishi ili kukidhi hali zao za maisha.
Alisema
uwepo na uingiaji wa wakimbizi nchini, umekuwa na mchango mkubwa katika
uzagaaji wa silaha haramu sanjari na kuongezeka kwa matukio ya utumiaji wa
silaha na kuathiri uchumi na maisha ya watu mbalimbali.
Katika hatua
nyingine, waziri huyo amesema serikali imefuta utaratibu wa kutoa uraia kwa
makundi, kama ilivyofanya kwa wakimbizi wa Burundi waliopo nchini. Alisema
kwamba kwa sasa uraia utatolewa kwa mtu kulingana na maombi yake.
Alisema
ukarimu huo wa Watanzania, umekuwa na athari kubwa katika ulinzi na usalama
nchini, hasa mikoa ambayo imewahifadhi watu hao kutokana na kuongezeka kwa
vitendo vya mauaji, ujambazi wa kutumia bunduki, lakini kupanda mbegu mbaya ya
kuuana kwa kulipiza visasi ambavyo vimekuwa vikifanywa na raia hao waliopewa
uraia.
“Kwa mamlaka
niliyopewa, natoa amri ya kusimamisha kutoa uraia kwa makundi kama ambavyo
imetoa Tanzania na haijawahi kutokea nchi nyingine, tumeona athari kubwa ya
watu hao na sasa sehemu kubwa ya Mkoa wa Tabora imekuwa na hali mbaya kiusalama
na tabia ya kulipizana visasi,” alieleza Mwigulu.
Akitoa
taarifa kwa waziri, Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi,
Marijani Nsato alisema silaha haramu 5,608 zikiwemo bunduki za kivita,
zilitarajia kuteketezwa. Nsato alisema katika silaha hizo, kulikuwa na bastola
21, Shortgun 606, SMG 166, Riffle 300, bastola bandia 21, FN Riffle 3, G3 moja,
SAR 3 na magobore 4487.
|
Sanjali na
bunduki hizo, aliitaja mikoa ambayo imeshiriki katika kuchangia bunduki haramu
zilizoteketezwa kuwa ni Kagera 100, Rukwa 189, Katavi 81, Simiyu 16, Mwanza 88,
Geita 82, Mara 80 na Kigoma ukiwa na jumla ya bunduki 424 ambazo zimeteketezwa
katika kazi ya jana.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga alisema mkoa huo kuwa mpakani na
kupokea idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu, kumechangia mkoa
huo kuathirika kwa kiasi kikubwa na uzagaaji silaha haramu na matukio ya
ujambazi kwa kutumia silaha.
Alisema mkoa
utaendelea kuweka mkakati wa kudhibiti silaha haramu na matukio ya ujambazi wa
kutumia silaha.
|
No comments:
Post a Comment