Moja ya
mradi wa maji uliodhamiwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited uliozinduliwa mapema Novemba mwaka jana
katika Kijiji cha Makanya wilayani Same katika
programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha.
Hapo,
Januari 24, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti imewapatia Watanzania zaidi
ya milioni mbili kote nchini maji safi
na salama bure katika kipindi cha miaka sita iliyopita kupitia programu ya hisani ya kusaidia jamii
inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga
kuboresha maisha.
Kupitia programu yake inayofahamika kama Maji
kwa Uhai, SBL imechimba visima vya kisasa 16 katika mikoa minane na kuwezesha
jamii katika maeneo hayo kupata maji ya uhakika na salama.
Akizungumza
katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma leo,January 25,2017 Mkurugenzi wa Mahusiano
wa SBL, John Wanyancha alisema kwamba
kampuni hiyo ya bia imejikita katika
kupunguza uhaba wa maji katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa
yakitaabika kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.
“SBL
ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu ambapo Maji ya
Maisha ikiwa ni moja ya maeneo manne ya
kipaumbele ambayo kampuni yetu
imeyafafanua katika malengo yake ya kutoa msaada kijamii kwa jamii
inamofanya shughuli zake, alisema Wanyancha akifafanua maeneo mengine ya kipaumbele kama Kutoa Stadi
za Maisha, Mazingira Endelevu na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.
|
Mkurugenzi
wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji ulioweza kuwafikia watanzania
milioni 2 katika programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni
hiyo inayolenga kuboresha maisha katika
mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema jana katika hoteli ya Morena Mkoani Dodoma.
Wanyancha
aliongeza kwamba kwa kutoa huduma ya maji ya uhakika katika jamii, SBL
imewawezesha watu kutumia muda mwingi zaidi katika uzalishaji kuliko kusafiri umbali mrefu kutafuta maji.
Aliongeza,
“licha ya kuboresha afya za wakazi wa maeneo hayo, upatikanaji wa maji safi na
salama ndani ya jamii unahakikisha kuwa
watoto hususani watoto wa kike wanaosoma
shule wanapata muda mzuri wa
kuhudhuria shuleni kwa uhuru
zaidi bila usumbufu”.
Mkurugenzi
huyo wa Mahusiano alieleza kwamba mpango
wa Maji ya Maisha kwa mwaka 2017 ni
kuanzisha miradi zaidi katika maeneo ya Ngare Nairobi, wilayani Siha,
Chang’ombe B wilayani Temeke (Dar es Salaam) na Karatu na Likamba katika mkoa
wa Arusha ambapo miradi yote itawanufaisha
wakazi zaidi ya 300,000.
|
No comments:
Post a Comment