Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA), Shabani Mdemu (kulia)
akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
|
Msemaji wa
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Ridhiwani Wema naye akizungumza jambo.
|
Mkutano na
wanahabari ukiendelea.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA), Shabani Mdemu leo
amekanusha taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii
hapa nchini kuwa madereva wamepanga kufanya mgomo Februari 26 mwaka huu akisema
taarifa hizo si za kweli na madereva wanapaswa kuzipuuza.
Naye Katibu
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Wasafirishaji kwa Njia ya Barabara, Salum
Abdallah alitoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za kuwepo kwa mgomo wa
madereva kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii na kuliomba Jeshi
la Polisi kuchukua hatua kwa wote waliohusika kusambaza taarifa hizo za
upotoshaji.
|
No comments:
Post a Comment