Ligi Taifa Daraja la 3 Mkoani Kagera ,kwa msimu huu wa 2017/2018 yanza rasmi Jumamosi January 07,2017-Bukoba na Karagwe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 08, 2017

Ligi Taifa Daraja la 3 Mkoani Kagera ,kwa msimu huu wa 2017/2018 yanza rasmi Jumamosi January 07,2017-Bukoba na Karagwe.

Kikosi cha Ngars Stars-Bingwa wa wilaya ya Ngara/2016/2017 kikiwa Uwanjani Kayanga/Karagwe kabla ya mchezo wake dhidi ya Nyaishozi FC.

Hatimaye  Ligi Taifa Daraja la 3  Mkoani Kagera ,kwa msimu huu wa 2017/2018 ,umeanza  rasmi Jana Jumamosi January 07,2017 katika Kituo cha Karagwe na Bukoba mjini huku  timu zilizopangwa   kuchea  uwanja wa  Kaitaba,katika mchezo wa Ufunguzi Timu ya Polisi Karagwe/Karagwe ilikubali kuchapwa bao 5-0 na Timu ya Majengo FC/Bukoba huku  Ngara  Boys/Ngara  ikichapwa  bao 3-2 na Muleba FC/Muleba,zote za Kundi A.

 Katika Kituo cha Karagwe/uwanja wa Kayanga aka Magufuli push up-Makamu Bingwa-Nzaza FC/Ngara ilikubali kutandikwa bao 2-0 na Eleven Stars/Misenyi huku Ngara Stars/Ngara ikiifunga 1-0 Nyaishozi FC/Karagwe.

Timu hizo zote zinatoka Kundi A
Suleiman Ally Kocha mkuu wa Ngara Stars na Benchi lake uwanja wa Kayanga/Karagwe.



Mashabiki uwanja wa Kayanga,wakifatilia mchezo .

Ligi hiyo inaendelea tena leo Jumapili January 08,2017 –uwanja wa Kaitaba/Bukoba kwa Kagera United/Manispaa dhidi ya Bingwa mtetezi-Murusagamba FC/Ngara huku mchezo wa saa 10 ukiwa kati ya Vatican FC/Muleba dhidi ya Halmashauri FC/Misenyi ,kutoka Kundi B.

Uwanja wa Kayanga /Karagwe-Benaco FC/Ngara  kucheza na Chandimu FC/Manispaa huku Atukuzwe FC/Karagwe dhidi ya Kamachumu FC/Muleba,zote kutoka Kundi B.

Salum Umande Chama-Katibu mkuu wa Chama cha soka Kagera KRFA(Suti ya kijivu) anaefata ni Katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Ngara-NDFA-Bahati Kunzi na wadau wengine wa soka wakifatilia michuano ya Ligi mkoa wa Kagera uwanja wa kayanga/Karagwe jana January 07,2017.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad