Taswira Picha 12 Lori la Mafuta aina ya Dizeli Likiteketea kwa moto wilayani Ngara/Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 22, 2016

Taswira Picha 12 Lori la Mafuta aina ya Dizeli Likiteketea kwa moto wilayani Ngara/Kagera.


Watu wawili wamenusulika kifo  baada ya Lori la Mafuta walilo kuwa wakisafiria  kupata hitilafu ya mfumo wa Umeme kwenye nyaya za gari hilo kisha kuwaka  moto na kuteketea kabisa katika eneo la Kumuyange wilayani Ngara mkoani Kagera.

Tukio hilo limetokea leo,September 22,2016  majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ikilihusisha gari aina ya SCANIA lenye namba za usajiri  za Burundi C0650A na tela lenye namba T 0587A  mali ya Kampuni ya VISIONI ya Ndikumana Gabliely raia wa Burundi  lililokuwalikitoka Dar es salaam kuekea Burundi.  


Lori hilo lilikuwa na Mafuta aina ya Dizeli lita 40,000 ambazo zote zimeteketea kwa moto huo.

 Licha ya Dereva na Tingo wake kutoka Salama katika Ajali hiyo, kwa kufanya zoezi la kuuzima moto huo kwa kutumia kifaa cha kuzimia moto, moto uliwashinda wakaamua kukimbia na kuliacha likiteketea.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad