Kilimanjaro Queens Mabingwa wa CECAFA 2016 upande wa Wanawake. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 20, 2016

Kilimanjaro Queens Mabingwa wa CECAFA 2016 upande wa Wanawake.

Timu ya Kilimanjaro Queens ya Tanzania bara ndio Mabingwa wa Cecafa upande wa kina dada 2016 baada ya kulaza Harambee Starlets wa Kenya 2-1.

 Fainali ya Mashindano ya CECAFA ya kugombea Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Kina dada iliyochezwa huko FUFA Technical Center, Njeru, Mjini Thika Nchini Uganda leo Septemba 20,2016 ambapo Magoli ya Tanzania yamefungwa na Mwahamisi Omar dk 28, 45, Kenya limefungwa na Christina Nafula.
Bao la Kenya, maarufu kama Harambee Starlets, lilifungwa Dakika ya 50 na Christine Nafula.

Kenya walifika fainali kwa kuwalaza Ethiopia 3-2.
Kilimanjaro Queens ilitinga Fainali kwa kuwatoa Wenyeji Uganda 4-1 na Harambee Starlets kuibwaga Ethiopia 3-2.

Kilimanjaro Queens, chini ya Kocha Sebastian Nkoma, walitoka Kundi B pamoja na Rwanda na Ethiopia, na wao kufuzu kama Washindi wa Kundi baada ya Kura ya Shilingi kufuatia kulingana kila kitu na Ethiopia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad