CAF MATAIFA YA AFRIKA U-17: SERENGETI BOYS WASONGA RAUNDI YA 3! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 22, 2016

CAF MATAIFA YA AFRIKA U-17: SERENGETI BOYS WASONGA RAUNDI YA 3!

Timu ya Taifa ya Vijana chini miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya timu ya Vijana ya Afrika Kusuni katika mchezo wa marudiano uliochezwa Jana Agosti 21,2016 kwenye uwanja wa Azam Complex kuwania kufuzu fainali za matifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo mashindano yanayotarajiwa kufanyika Madagascar.

Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na  Mohamed Abdala aliyefunga dakika ya 34 kipindi cha kwanza wakati bao la pili likifungwa dakika za lala salama na Muhsin Makame.

Serengeti Boys imeitupa nje timu ya taifa ya Afrika Kusini kwa jumla ya magoli 3-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa awali uliopigwa Afrika Kusini.
Kwenye Raundi ya 3, Serengeti watacheza na Mshindi kati ya Namibia na Congo Brazzaville na Mshindi wa hapo moja kwa moja anaenda Fainali ambazo zitakuwa na Nchi 8.

September mwaka huu,2016, Serengeti Boys itakuwa mwenyeji wa Namibia au Congo Brazzaville huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa mwezi October.

Fainali za Mashindano haya zitachezwa huko Nchini Madagascar kati ya Aprili 2 na 16 Mwakani 2017 na Timu ambazo zitafika Nusu Fainali za Mashindano hayo watakwenda kucheza Fainali za FIFA Kombe la Dunia U-17 huko India Mwakani 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad