TAZAMA PICHA/HABARI:-Ni Gari la Kifahari Lililotengeneza na Kijana wa Kitanzania na Kuitwa..‘KAPARATA’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 08, 2016

TAZAMA PICHA/HABARI:-Ni Gari la Kifahari Lililotengeneza na Kijana wa Kitanzania na Kuitwa..‘KAPARATA’

Kijana Jacob Louis 'Kaparata' (38) akiwa ndani ya gari lake la Kifahari alilolitengeneza  aina ya 'Kaparata' kwa kipindi cha miezi mitatu tu katika viwanja vya maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) jijini Dar es Salaam.


SIYO Jeep la Mmarekani wala Korando la Mkorea. Hili ni gari aina ya Kaparata ambalo limebuniwa na kutengenezwa na kijana Mtanzania, Jacob Louis ‘Kaparata’ (38), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambaye ametumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa hapa nchini.

Waliobahatika kuliona gari hili katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa – Saba Saba wamekiri kwamba huu ni ubunifu mkubwa ambao unastahili kuungwa mkono na serikali na mamlaka nyingine.


Nimetumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa nchini. Chassis nimeitengeneza kwa kutumia square pipe, bodi nimelisuka kwa kutumia brake pipes zinazotumika kutengenezea vitanda na nikatumia mabati ya gauge 18 ambayo yanatumika kutengenezea mageti,” anafafanua Kaparata.

Anaongeza: “Nilipomaliza kutengeneza chassis nikaenda kununua injini, diff, gear box na matairi, ambavyo vyote ni vya gari aina ya Suzuki Carry. Unajua Suzuki Carry ni fupi ina futi 10, lakini nilichokifanya ni kuongeza chassis hadi futi 12

Injini ina nguvu sana ila kigari kile kimenyimwa bodi. Sasa gari yangu hii imeonekana kuwa na nguvu, ina kasi.

Kaparata anasema kwamba, gari yake ina muundo wa kipekee tofauti na gari lolote duniani na ameitengeneza kwa kipindi cha miezi mitatu tu kabla ya maonyesho ya mwaka huu ya Saba Saba ambapo limemgharimu kiasi cha Shs. 12,850,000.


Jacob Louis 'Kaparata' akiingia kwenye gari lake alilolitengeneza mwenyewe kwa miezi mitatu.


Nilipokuwa mdogo nilikuwa mtundu sana nikitengeneza magari na vitu mbalimbali kwa kuiga nilivyoviona, ndipo watoto wenzangu wakanipachika jina la ‘Kaparata’, ambalo nimelizowea na kuamua kuiita kampuni yangu kwa jina hilo.

“Tangu mdogo nilipenda kuangalia filamu na nilivutiwa na gari moja nililoliona kwenye filamu ya Delta Force ya Chuck Norris (The Flyer 72 Advanced Light Strike Vehicle) nikaapa kwamba lazima nije nitengeneze gari la aina hiyo,” anasema Kaparata.

Hata hivyo, anasema kwamba, alitumia muda wa wiki mbili kutengeneza chassis ambayo alihakikisha inanyooka na kukaa sawa kabla ya kuendelea na utundu mwingine.

“Hivi sasa nikitembea na gari yangu, hata kama tumeongozana na magari mengine ya kifahari, watu wataitazama gari yangu mitaani na wamevutiwa nayo huku wengine wakinitaka nitengeneze mengine niyauze,” anasema.

Anasema wakati anaanza kuitengeneza gari hiyo vifaa pekee alivyokuwa navyo ni drill machine, grander na welding machine – vifaa vitatu tu, ambapo mabati na vifaa vingine alivinunua.

Kwa kuwa yeye si fundi mchundo, mabati na vifaa vingine aliyapeleka kwa mafundi mchundo ambao walimkunjia kwa muundo na vipimo alivyovitaka yeye.

Lakini nimeingia hasara kubwa kwa sababu wakati mwingine unampelekea mtu akukunjie bomba au bati, lakini anakosea, inabidi kulitupa na kutafuta jingine.....BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI HABARI HII.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad