|
Joshua Kimmich
aligongesha mwamba kwa upande wa Ujerumani huku golikipa wa Ufaransa Hugo
Lloris akiokoa mchomo wa hatari kuwanyima goli washindi hao wa kombe la dunia.
Rekodi zilizowekwa
baada ya mchezo huo.
Ufaransa ni nchi ya kwanza kufika fainali
ya Euro ikiwa nchi mwenyeji wa mashindano (mara ya kwanza ilikuwa 1984)
Ufaransa wamefunga Ujerumani kwenye
michuano mikubwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958. Ni mchezo wao wa kwanza
pia kutoruhusu goli dhidi ya Ujerumani.
Ujerumani wamepoteza nusu fainali yao ya
nne kati ya sita kwenye michuano mikubwa (2006, 2010, 2012, 2016).
Bastian Schweinsteiger amecheza mchezo wake
wa 38 kwenye michuano mikubwa, michezo mingi zaidi ya mchezaji yeyote kwenye
historia ya Kombe la Dunia na michuano ya Ulaya.
Michel Platini bado anashikilia rekodi ya
magoli mengi zaidi kwenye msimu mmoja wa michuano ya Euro (magoli 9 Euro 1984)
magoli matatu zaidi ya Antoine Griezmann aliyefunga magoli 6 hadi sasa Euro
2016
|
No comments:
Post a Comment