TASWIRA PICHA/AJALI:-Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo....Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 27, 2016

TASWIRA PICHA/AJALI:-Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo....Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa.

Basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, July 27,2016, wakati Basi hilo likotokea stendi ya Gerezani, Kariakoo kuelekea Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana ,” amesema Kaimu kamanda huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad