|
Wakuu wa Wilaya wateule saba wa Wilaya za Mkoa wa Kagera
wameapishwa rasmi leo Julai 4, 2016 na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja
Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Kagera.
Wakuu hao saba wa
Wilaya waliapa mbele ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu kwa kula viapo vitatu ambavyo
ni Kiapo cha Utii, Kiapo cha Utumishi na Kiapo cha kutunza siri za Serikali.
Aidha, tayari wamekula Kiapo cha Maadili mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli tarehe 29/06/2016 ikiwa ni pamoja na
kupokea maelekezo ya utekelezaji wa shughuli zao.
Mara baada ya kula
viapo vyao Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu aliwapongeza kwa kuteuliwa kuwa Wakuu wa
Wilaya wapya wa wilaya za Mkoa wa Kagera pia akawaasa kufanya kazi zao kwa
kuzingatia Kauli mbiu ya Mhe. Rais Magufuli
ya “Hapa Kazi tu”
|
No comments:
Post a Comment