SIMANZI / PICHA:- Watu 29 wafariki dunia ajalini mkoani Singida leo Julai 04,2016… Rais Magufuli atuma salamu za pole kwa waliofiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 04, 2016

SIMANZI / PICHA:- Watu 29 wafariki dunia ajalini mkoani Singida leo Julai 04,2016… Rais Magufuli atuma salamu za pole kwa waliofiwa.

Watu 29 wamefariki dunia kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha mabasi mawili mali ya kampuni moja ya City Boy, ambayo yaligongana uso kwa uso katika kijiji cha Maweni, tarafa ya Kintinku, wilayani Manyoni, mkoa wa Singida.

Ajali hiyo iliyotokea saa tisa alasiri ya leo,Julai 04,2016 imehusisha basi namba T 531 DCE, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Kahama, na jingine lenye namba za usajili T 247 DCD, lililokuwa likitokea Kahama kuelekea Dar es salaam.

 Mabasi hayo yaligongana wakati yakiwa yanapishana.


Taarifa za awali zinaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni mwendo kasi, kwani kabla ya tukio, moja ya mabasi hayo, lenye namba za usajili T 247 DCD, lilikamatwa na dereva wake kupigwa faini ya shilingi 30,000/= kwa mujibu wa sheria. 

Basi hilo lilikamatwa likiwa katika mwendo kasi wa km 122 kwa saa. kama inavyoonekana katika picha ya awali hapo juu.

Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.


Pichani ni hali ilivyokuwa katika eneo la tukio.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad