TASWIRA PICHA :-Rais Magufuli na rekodi aliyoivunja Kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya wa CCM. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 24, 2016

TASWIRA PICHA :-Rais Magufuli na rekodi aliyoivunja Kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya wa CCM.


Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo July 23, 2016,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi (CCM),Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika.


Makamu Mwenyekiti-Zanzibar Dkt Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10,pichani katia anaeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhamani Kinana akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.

Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya Wajumbe wa Mkutano mkuu Maalum wa chama cha CCM mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho.


Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavunja rekodi baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa kwa kupata asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa.



Rekodi hiyo ya kupata asilimia 100 ya kura zote kwenye uchaguzi wa aina hiyo (Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa) haijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote ndani ya CCM tangu kuanzishwa kwa chama hico Februari 05, 1977 ambapo ni miaka 39 sasa.



Wenyeviti wa CCM waliyopita ambao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa wala Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete hawakuwahi kupata kura zote zilizopigwa kwenye uchaguzi wa ngazi hiyo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliyofanyika mjini Dodoma leo,July 23,2016 Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema matokeo kuwa;
ifuatavyo

Kura zilizopigwa zilikuwa ni 2398


Kura halali ni 2398


Kura zilizoharibika ni 0, kura za hapana ni 0 na kura za Ndiyo ni 2398.

Baada ya kumtangaza mshindi, Dkt. Kikwete alimkabidhi Mwenyekiti mpya Dkt. Magufuli nyaraka za uongozi na baada ya hapo Dkt. Kikwete alitangaza kustaafu rasmi Uenyekiti wa CCM na kumuachia Dkt. Magufuli aongoze kwa miaka mitano ijayo.
 





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad