TASWIRA PICHA 7:- Za Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Ngara leo July 23, 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 23, 2016

TASWIRA PICHA 7:- Za Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Ngara leo July 23, 2016.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu  atapokea Mwenge huo kutoka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma , Brigedia Jenerali Emanuel Maganga leo Jumamosi July 23, 2016, katika Wilaya Ngara Kata ya Murusagamba mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Kagera ambapo  Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Mkoani Kagera katika Halmshauri zote  za Wilaya Saba na Manispaa ya Bukoba na kupitia jumla ya miradi 68.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Mhe. Lt.Col. Michael Mangwela Mntenjele Kushoto akiupokea Mwenge wa uhuru wilayani Ngara leo July 23, 2016.

Mwenge huo utatembelea miradi ya maendeleo  9 yenye jumla ya Shilingi Bilioni 1.95 kutoka sekta ya Elimu,Afya,Maji ,Kilimo ,Ufugaji,Uvuvi,Ardhi na Mazingira pamoja na miradi ya watu binafsi ,itawekewa jiwe la msingi,kuzinduliwa , kufunguliwa na kukaguliwa.


Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Mhe. Lt.Col. Michael Mangwela Mntenjele akiwa na Viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mara baada ya kuzindua mradi wa Maji katika Kijiji cha Rwinyana wilayani wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Ngara leo July 23, 2016.


Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ni “Vijna ni Nguvukazi ya Taifa Washirikishwe na kuwezeshwa.Tujenge Jamii Maisha na Utu Wetu; Bila Dawa za Kulevya; Tanzania bila Maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI; Inawezekana; Timiza wajibu wako kata mnyororo wa rushwa; Wekeza katika Maisha ya baadae; Tokomeza Malaria.
Katika Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru utapokelewa Wilayani Ngara tarehe 23/07/2016 na makabidhiano baada ya Ngara, Karagwe, Kyerwa, Misenyi, Bukoba Vijijini, Manispaa ya Bukoba, Muleba na mwisho ni Wilaya ya Biharamulo na Mkoa utakabidhi Mwenge Mkoa wa Geita.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad