Kamanda Matei alisema
kati ya majeruhi hao, sita hali zao ni mbaya na walikimbizwa katika Hospitali
ya Rufaa ya Morogoro kupatiwa matibabu zaidi.
Alisema ajali hiyo ilitokea saa
10 alfajiri ya Julai Mosi mwaka huu,2016 wakati basi hilo likitokea Bukoba mkoani
Kagera kwenda Dar es Salaam.
Waliokufa katika ajali
hiyo kwa mujibu wa Kamanda Matei ni dereva wa basi hilo, msaidizi wake,
kondakta na abiria wengine watatu.
Alitaja majina ya
waliokufa kuwa ni Yassin Mgongolwa (41) dereva wa basi hilo, Veronica Jeremia
ambaye ni kondakta, Said Shomari Simba (30) dereva msaidizi na abiria Lilian
Paul (34), Jonia Kokumbuga na mwamamke mwingine mwenye umri kati ya miaka 30
-35, ambaye hajatambulika.
Miili ya marehemu hao
na maiti zilizoungua na kushindwa kutambuliwa, imehifadhiwa katika chumba cha
maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.
Kamanda Matei alisema
kabla ya basi hilo kupata ajali, lilisimamishwa na askari wa usalama
barabarani, lakini dereva alikaidi na kupitiliza na baada ya muda likapata
ajali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Dk Stephen Kebwe, ambaye pia alifika eneo la tukio hilo jana, alisema
miili iliyoungua, itatambuliwa kwa kutumia vinasaba (DNA) na kuwataka ndugu na
jamaa zao kuwa na subira wakati utambuzi huo utakapofanyika.
Alilipongeza Jeshi la
Polisi mkoa na vikosi vya Zimamoto na wananchi wa vijiji vya karibu na eneo la
ajali kwa kusaidia kuzima moto na kuokoa majeruhi wa ajali hiyo.
|
No comments:
Post a Comment