TASWIRA PICHA:-Watu 5 wamefariki Dunia na 35 wamejeruhiwa katika ajali ya Basi mkoani Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 20, 2016

TASWIRA PICHA:-Watu 5 wamefariki Dunia na 35 wamejeruhiwa katika ajali ya Basi mkoani Morogoro.

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine 35 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya NBS lenye namba za usajili T 909 BXK lililo kuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda Mkoani Tabora kuanguka leo June 20,2016 katika eneo la Tabu Hotel kata ya Chigela wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Mganga wa hospitali ya wilaya ya Gairo,Bw. Mushi Mabula amethibitisha kupokea maiti tano na majeruhi 26 ambapo amesema watu saba hali zao sinzuri na watahamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
  
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakilazwa katika hospitali ya wilaya ya Gairo.
Basi la KISBO lilivyopata ajali.

Ajali nyingine ni ya basi la Kampuni ya KISBO lenye namba za Usajili T 895 CYL lililopata ajali maeneo ya Dumira Morogoro, kwa kuparuzana na trailer Flatbed na hakuna mtu aliyeripotiwa kufariki japo kuna majruhi kadhaa.

Akithibitisha ajali hiyo, Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Leonce Rwegasira amesema, ajali hiyo imetokea majira ya saa tano asubuhi huku chanzo chake kikidaiwa kuwa ni mwendokasi wa dereva wa basi.

Kamanda Rwegasira ametaja baadhi ya majina ya marehemu kuwa ni Salmin Shabani mkazi wa urambo, Clement Mpondi mwenye umri kati ya miaka 40-50, wanawake wawili ambao majina yao hayakuweza kutambulika mara moja na mtoto anayekadiriwa kuwa na miezi sita hadi minane ambaye alikuwa amebebwa  na mama yake.

Basi la NBS lilivyopata ajali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad