TASWIRA PICHA:- Mama Janeth Magufuli aahidi kuendelea kusaidia Jamii ya Wazee na Walemavu Nchini Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 03, 2016

TASWIRA PICHA:- Mama Janeth Magufuli aahidi kuendelea kusaidia Jamii ya Wazee na Walemavu Nchini Tanzania.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli(kushoto) akikabidhi misaada kwa wawakilishi wa kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na kuahidi kuendelea kusaidia kambi hizo za wazee na watu wenye ulemavu wa ukoma ambapo mpaka sasa meshatoa msaada katika kambi 4 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara yenye thamani ya Takribani shilingi 250.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi kutoka wawakilishi wa kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya watoto waliofika katika hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiagana na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi baada ya kutoa msaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo eneo hilo. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.BOFYA HAPA KUTAZAMA PICHA ZAIDI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad