TANAPA:-Na Ujenzi wa Miundombinu Maeneo yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Mahale Mkoani Kgoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2016

TANAPA:-Na Ujenzi wa Miundombinu Maeneo yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Mahale Mkoani Kgoma.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kuta tatua changamoto ya wananchi katka vijiji hivyo kuvuka kwenda upande mwingine ambako kwa sasa wamekuwa wakilazimika kuvuka katikati ya mto huku wakiwa wamebeba vyombo vyao vya usafiri na hata mifugo imekua ikipita katika mto huo.


Picha juu na chini ni Baadhi ya mafundi wakijaribu kuchimba udongo katika eneo la mto Lagosa ambako daraja hilo linajengwa.

Wanahabari wakimsilikiliza Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Lilangela inayojenga daraja la Lagosa katika barabara ya Buhingu wilayani Uvinza ,Marango Ngose alipokuwa akizungumzia juu ya ujenzi huo unaofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Baadhi ya malighafi zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zikiwa eneo la ujenzi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyeko Kigoma.

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetoa Sh. Milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ikiwa ni njia moja ya kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Milima ya Mahale vilivyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. 

Baadhi ya Wananchi wanaoishi katika vijiji vya Lukoma na Igalula wanakabiliwa na changamoto ya barabara jambo linalowafanya washindwe kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea vijiji hivyo vilivyoko mwambao mwa zimwa Tanganyika, Mkuu wa idara ya ujirani mwema ,Mhifadhi Romanus Mkonda aliyataja madaraja hayo kuwa Lagosa na Lukoma.

Daraja la Lagosa linatumia Sh. Milioni 296 wakati lile la Lukoma litatumia Sh. Milioni 288,” alisema.

Alisema lengo la TANAPA ni kusaidia jitihada za serikali za kuimarisha mawasiliano ya barabara katika ukanda huo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17, TANAPA imetenga Sh. Milioni 500 kwa ajili ya kujenga madaraja ya Nkonkwa na Igalula yaliyopo vijijini hapo.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Igalula, Mussa Matililo alisema iwapo madaraja hao yatakamilika itawarahisishia wananchi wa maeneo hayo katika shughuli zao za kilimo...SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad