MAONESHO YA SABASABA:- RC Makonda atembelea banda la Umoja wa Mataifa UN. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2016

MAONESHO YA SABASABA:- RC Makonda atembelea banda la Umoja wa Mataifa UN.

Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Makonda alifika katika banda hilo na kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa UN kuhusu kazi ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa nchini.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) yaliyobandikwa katika banda la UN na jinsi walivyojipanga katika kuelimisha wananchi kuhusiana na malengo hayo kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu katika picha ya pamoja huku wakiwa na bango maalum linalowakilisha rangi za malengo 17 ya SDGs na mmoja wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo kwenye ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Wananchi mbalimbali wakiingia katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa kwa ajili ya kujipatia bidhaa mbalimbali. Maonyesho hayo yameanza jana jijini Dar es salaam.....TAZAMA MATUKIO PICHA ZIDI KWA KUBOFYA HAPA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad