ROBO FAINALI EURO 2016:- LEWANDOWKSKI v/s RONALDO-(Poland na Ureno) - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 30, 2016

ROBO FAINALI EURO 2016:- LEWANDOWKSKI v/s RONALDO-(Poland na Ureno)

Poland na Ureno leo, June 30, 2016 wanakutana katika mchezo wa robo fainali ya kwanza kabisa katika michuano ya Euro mwaka huu, mchezo utakaofanyika kunako dimba la Stade Vélodrome lililopo jijini Marseille.

William Carvalho, Pepe na Ricardo Quaresma  wote kwa pamoja wana kadi za njano na ikiwa leo watapata kadi nyingine na timu yao kufuzu hatua ya nusu fainali basi wataukosa mchezo huo.

Vivyo hivyo kwa upande wa Poland,  Kamil Grosicki, Artur Jedrzejczyk, Krzysztof Maczynski, Michal Pazdan, Slawomir Peszko, Lukasz Piszczek wote wana kadi za njano.

Takwmu za michezo waliyokutana.

  • Hii inakuwa ni mara ya tatu kati ya Poland na Ureno katika michuano mbalimbali. 

  • Poland walishinda 1-0 mwaka 1986 katika fainali za Kombe la Dunia na baadaye Ureno kushinda 4-0 katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002.

  • Poland hawajapoteza dhidi ya Ureno katika michezo yao mitatu ya mwisho (wameshinda mara moja, wametoka sare mara mbili).

  • Mara ya mwisho kukutana, timu hizi zilitoka sare ya 0-0, mchezo uliofanyika Warsaw mwaka 2012.

 Kuanzia Ijumaa hadi Jumapili kila Siku itachezwa Mechi moja za Mechi zilizobaki za Robo Fainali.

Wales v Belgium (Ijumaa,Julai 01,2016 Saa 4 Usiku)

Germany v Italy (Jumamosi,Julai 02,2016 Saa 4 Usiku)

France v Iceland (Jumapili,Julai 03,2016 Saa 4 Usiku)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad