MATUKIO PICHA:-Tanzania Yapongezwa kwa ukarimu wa Kuwahifadhi Wakimbizi kwa zaidi ya Miongo Minne. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 21, 2016

MATUKIO PICHA:-Tanzania Yapongezwa kwa ukarimu wa Kuwahifadhi Wakimbizi kwa zaidi ya Miongo Minne.

Maandamano ya wakimbizi yakiingia uwanjani katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. (Picha na story Modewjiblog).
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akisoma risala wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Katika hatua nyingine,Nchi ya  Tanzania imepongezwa kwa ukarimu wake kwa kuwahifadhi wakimbizi kwa zaidi ya miongo minne sio tu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hata duniani.

Mwakilishi mkazi wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Chansa Kapaya alisema hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani yenye kauli mbiu kuwa “Tupo Pamoja na Wakimbizi, Tafadhali ungana nasi”.
Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa mfano mzuri wa kuwahifadhi wakimbizi wengi duniani na pia kuwatafutia suluhu,” alisema.

Alisema mwaka 2014 Tanzania iliwapa uraia wakimbizi zaidia ya 162,000 baada ya kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 40.

Aliongeza kuwa, wakimbizi wanapaswa kuthaminiwa kama binadamu wengine kwa kuwa hakuna mtu anayechagua kuwa mkimbizi.

Kapaya alisema kuwa kwa sasa kambi ya Nyarugusu ina wakimbizi zaidi ya 131,733 ambao ni wengi zaidi na kusababisha msongamano unaohatarisha maisha yao.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga (kulia) akifurahi jambo na  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita wakati burudani mbalimbali zikiendelea kwenye maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akiteta jambo na Ofisa wa UNHCR Tanzania anayeshughulika na mambo ya usalama kambini, David Mulbah (kulia) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyobeba kauli mbiu “Tupo Pamoja na wakimbizi. Tafadhali ungana nasi.”  ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya kwa pamoja wakikabidhi jezi na zawadi kwa timu wakimbizi ya vijana ya wanawake ya mpira wa miguu katika maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya kwa pamoja wakikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wakimbizi waliofanya vizuri kwenye masomo yao.


Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner akitoa neno la kufunga sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akiongozwa na Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, Sospeter Boyo (kulia) kutembelea mabanda yenye bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa mikono na vikundi mbalimbali vya wakimbizi wanaoishi kwenye kambi hiyo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.


Juu ni Mabinti wa Congo DRC na chini Mabinti wa Kirundi wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad