KUFUZU FAINALI ZA VIJANA MADAGASCAR:- Serengeti Boys yaitwanga Shelisheli mabao 3-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 26, 2016

KUFUZU FAINALI ZA VIJANA MADAGASCAR:- Serengeti Boys yaitwanga Shelisheli mabao 3-0.

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeanza vema katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza ya kufuzu Fainali za Vijana chini ya miaka 17  Afrika mwakani Madagascar baada ya kuitwanga Shelisheli kwa mabao 3-0.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo June 26, 2016, Segengeti Boys ingeweza kupata mabao mengi zaidi kama washambuliaji wake wangekuwa makini.
Magoli ya timu hiyo yalifungwa na Shaaban Zubeiry Ada dakika ya 15, Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 22 huku bao la tatu lililofungwa kwa penalti na beki wa kati Ally Hussein Msengi dakika ya 62, baada ya beki wa Shelisheli, Stan Esther kuunawa mpira wa adhabu wa Asad Ali Juma katika ukuta.

Baada ya ushindi huo, Serengeti Boys itahitaji kwenda kulazimisha sare kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo Shelisheli ili kukata tiketi ya kwenda kukutana na Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad