EURO 2016:-Ubelgiji yatinga robo fainali..Leo ni Italia na Hispania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 27, 2016

EURO 2016:-Ubelgiji yatinga robo fainali..Leo ni Italia na Hispania.

Jana June 26, 2016 ,Katika michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa, Ubelgiji imeichabanga Hungary 4-0 na kufanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Mapema Ujerumani waliichapa Slovakia 3-0 huku wenyeji Ufaransa wakishinda 2-1 dhidi ya Jamuhuri ya Ireland.
Mshambuliaji wa Ubelgiji, Eden Hazard akishangilia baada ya kuifungia timu yake katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Hungary kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora Euro 2016 Uwanja wa Manisipaa mjini Toulouse, Ufaransa,Jana Jne 26,2016.
 Mabao mengine ya Ubelgiji yamefungwa na Toby Alderweireld, Michy Batshuayi naYannick Carrasco na Ubelgiji inakwenda Robo Fainali ambako itakutana na Wales.
Michuano hiyo itaendelea tena leo,June 27, 2016 ambapo Mabingwa wa zamani wa Dunia Italia watapambana na miamba ya soka Uhispania huku mtanange mwingine ukiwa baina ya Uingereza dhidi ya Iceland.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad