CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC yalizwa tena na Miamba ya Afrika TP Mazembe ya Congo DR. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC yalizwa tena na Miamba ya Afrika TP Mazembe ya Congo DR.

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, Leo June 28, 2016 wakicheza Nyumbani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambao ulifurika kupindukia baada ya Mashabiki kuingia bure bila malipo wamepoteza Mechi yao ya pili mfululizo ya Kundi A la Mashindano ya Klabu Barani Afrika ya CAF KOMBE LA SHIRIKISHO kwa kupigwa 1-0 na Miamba ya Afrika TP Mazembe ya Congo DR.

Yanga SC walianza kwa kufungwa 1-0 Ugenini huko Algeria walipofungwa na MO Bejaia na Mechi yao inayofuata, ikiwa ya 3 kwa Kundi A, ni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam hapo Julai 15,2016 dhidi ya Medeama ya Ghana.
Bao lililoiua Yanga SC hii Leo lilifungwa Dakika ya 75 na Merveille Bope.   
     
Mechi nyingine ya Kundi A ni Jumatano Juni 29 wakati Medeama wakiwa kwao Ghana kucheza na MO Bejaia ya Algeria.

Kwenye Kundi A, TP Mazembe wako kileleni baada ya kushinda Mechi zao zote mbili wakiwa na Pointi 6 na Yanga SC wako mkiani wakiwa hawana Pointi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad