BIASHARA:-Wafanyabiashara wa Mpunga Kahama/Shinyang'a waonywa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 19, 2016

BIASHARA:-Wafanyabiashara wa Mpunga Kahama/Shinyang'a waonywa.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,Bw. Vita Kawawa amewapiga marufuku wafanyabiashara kusafirisha mpunga bila ya kukobolewa nje ya wilaya hiyo ili kunusuru viwanda kufungwa na vijana kukosa ajira.

Bw.Kawawa amesema amri hiyo inalenga kuongeza fursa za ajira kwa vijana na mapato kwa viwanda hivyo vya kukoboa mpunga na wafanyabiashara wanaowekeza katika biashara hiyo.

 “Kahama kuna zaidi ya viwanda 140 vya kukoboa mpunga na vimeajiri wafanyakazi 4,100 na wanaofanya kazi za kupepeta mchele 2,500, hivyo kununua mpunga na kuusafirisha nje ya wilaya bila kuukoboa ni kuviua viwanda hivyo na kukosesha ajira watu zaidi ya 6,000 wanaonufaika na uwapo wa viwanda vya kukoboa mpunga,” amesema Kawawa...SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad